JESHI MOJA: Tunaliona ni Jeshi linalomwinua Mungu na Kujazwa na Roho katika Karne ya 21 – tukijisadikisha na wito wetu, Twende Mbele Pamoja.

Tuta...

 • zama ndani zaidi katika maisha yetu ya Kiroho
 • ungana kwa Maombi
 • watambua na kuwaendeleza viongozi
 • ongeza hali ya kijitegemea na kujinyima

MISHENI MOJA: Katika ulimwengu wa watesekao, waliokata tamaa, wapweke, walioporwa na kupoteza, kuwakia kwa Upendo kwa njia yoyote ile

Tuta...

 • sisitiza huduma yetu ya mchangamano
 • wakia na kuwahusisha Vijana na watoto
 • watetea na kuwahuduma wasiojiweza
 • kutia moyo uvumbuzi katika Misheni

UJUMBE MMOJA: Kwa ujumbe wa Yesu wenye kufanya Mabadiliko, unaoleta uhuru, tumaini na uzima

Tuta...

 • mwasilisha Kristo bila aibu
 • thibitisha imani yetu katika mabadiliko
 • fanya uinjilisti na ufuasi kwa mafanikio
 • toa nyezo bora za kufundishia

Rasilimali